Mchekeshaji maarufu Bongo, Joseph Senga ‘Senga’ amefunguka kuwa busu alilompiga staa wa kike wa filamu, Kajala Masanja lilimfanya alale usingizi mnono sana ukizingatia kuwa hajawahi kubusu shavu laini kiasi hicho kwasababu warembo wengi wanazingua.
Akizungumza na Centre Spread, Senga alisema alipata fursa hiyo ya kumpiga busu wakati wakiigiza filamu matata ya Pishu iliyoandaliwa na Kajala Entertainment, itakayoingia sokoni Mei Mosi, ambapo alisema anajikubali katika filamu hiyo ambayo anaamini itavunja watu mbavu.
“Wewewee umpige busu Kajala utashindwa kulala kweli jamani,yaani nilishtuka kumeshakucha kabisa lakini pamoja na yote mimi ni mchekeshaji ila kwa filamu ya Pishu nimeinua mikono,” alisema Senga.