Kwa sasa ACT-Wazalendo ni Zitto Kabwe, bila Zitto Kabwe hata uhai wa ACT-Wazalendo haupo!.
Ziara ya Viongozi wakuu wa ACT-Wazalendo katika mikoa ya Ruvuma, Njombe, Iringa, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mara na Mwanza imeangaza picha na kutoa majibu mengi.
Ni ukweli kuwa, kuingia kwa ACT-Wazalendo kwenye uwanja wa siasa nchini umewatikisa UKAWA na unaifanya CCM kujitathmini na kuwa waangalifu katika mchakato wa kuwapata wagombea wake.Kabla ya ACT-Wazalendo, nguvu ya kisiasa ilikuwa mikononi mwa CCM na UKAWA.
ACT-Wazalendo unaifanya UKAWA kukosa kwa kiwango kikubwa umuhimu wa Muungano wao kama nia yao ni kutaka kuunganisha idadi ya kura ili kuishinda CCM na siyo kuunganisha philosophy, policies and manifesto.
ACT-Wazalendo unaifanya CCM kuachana na politics as usual katika mchakato wa kupata wagombea kwa sababu ACT-Wazalendo ni zaidi ya Independent candidate katika nguvu za CCM. CCM wangeweza kuendelea kufanya politics as usual kama nguvu ya kisiasa ingebakia ni UKAWA pekee kwa sababu wale wangefanyiwa vitimbwi ndani ya CCM wasingepata nafasi tena ya kukimbilia UKAWA na kupata nafasi ya kuwa wagombea kwa sababu muungano wa UKAWA umeishafukia nafasi tatu kati ya nne za wagombea kutoka vyama vinavyounda muungano wa UKAWA kuanzia udiwani, Ubunge mpaka Urais.
ACT-Wazalendo imeingia kwenye uwanja wa siasa na clear-cut central idea and programme soundly ikisaidiwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vingi vya mawasiliano nchini kwa sababu imebeba majibu ya mapungufu ya UKAWA na CCM katika siasa za Tanzania lakini kikubwa zaidi, inafanya siasa zake nje ya confrontational environment ukilinganisha na vyama vikubwa hasa ikichukuliwa kuwa, Watanzania wengi hawapendi siasa za vurugu.
Wananchi wengi watakaojiunga na ACT-Wazalendo kutoka CCM watakuwa ni wale wanaamini CCM imeacha misingi ya uanzishwaji wake na vile vile rushwa imekuwa ni kigezo cha kupata uongozi ndani ya chama na serikali yake.
Wananchi wengi watakaojiunga na ACT-Wazalendo kutoka UKAWA watakuwa ni wale wanaamini Muungano wa CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD umewanyima demokrasia ya kuchaguliwa ndani ya vyama vyao baada ya kuwekesha nguvu na pesa katika vyama hivyo na pia kuna wengine watafanya hivyo kwa sababu wanaamini ni wahanga wa uongozi wenye hekima na busara za makengeza.
Ninaamini huu ni ukweli unaonekana na wachache kwa kutumia naked eye na katika ukweli huu, ndiyo nguvu ya ACT-Wazalendo kupitia kwa Zitto Kabwe inakuwa ni power broker.
Ni wajinga na wapumbavu watakaopuuza na kubeza uwepo wa ACT-Wazalendo iliyo chini ya Zitto Kabwe katika mstakabali wa chaguzi za Tanzania Bara katika mazingira ya siasa za ndani ya UKAWA na CCM.
Kuna baadhi ya wananchi wameanza kuja na hoja nyepesi za kisiasa kuhusiana na ujio wa ACT-Wazalendo wakiamini ni hoja mbadala au ni hoja zinazotuliza ombwe lao la fikra pevu.
Kuna baadhi ya wananchi wameanza kudai eti haka ni kachama kadogo. Fine!.
Hoja ya msingi hapa, Ziara walizofanya katika mikoa kumi imetoa majibu ya maana ya ''haka kachama kadogo''.
Kuna baadhi wanadai ACT-Wazalendo ni chama cha wasaliti. Fine!.
Hoja ya msingi hapa, wasaliti wa nani katika taifa Iinalokadiriwa na National Bureau of Statistics (NBS) office kuwa ifikapo siku ya uchaguzi, Tanzania itakuwa na watu wapatao 48,522,228, ambapo watakaokuwa na umri wa kupiga kura mwaka huu watakuwa ni watu 24,253,541.
Kuna wengine wanadai, ACT-Wazalendo ni tawi la CCM. Fine!.
Hoja ya msingi hapa, vyama vingine ni matawi ya nani kwa faida ya nani?
Kuna wengine pia wanakuja na hoja wakisema, ACT-Wazalendo imekuja kugawa kura za UKAWA. Fine!.
Hoja ya msingi hapa, kura hazigawanywi kama njugu. Kinachogawa kura ni philosophy, policies and manifesto, labda kama misingi hii ya ACT-Wazalendo inafanana na UKAWA lakini kikubwa zaidi, Tanzania hivi sasa ina zaidi ya vyama 22 vyenye usajili wa kudumu chini ya Rais aliyechaguliwa na wananchi 5,276,827 kati ya wananchi 20,137,303 waliojiandikisha kupiga kura.
Wahenga walisema, ‘Mchelea mwana kulia hulia yeye’ na ‘Mdharau mwiba mguu huota tende’ lakini kwa wale wanafahamu maana yake, this is an opportunity to step back, reflect and refocus.
Kwa mtaji huu, ACT-Wazalendo is a force to be reckoned with. Be prepared to deal with any mischief.
By Ng'wamapalala