Baada ya ile story iliyozagaa mitandaoni kuwa mwanadada Amanda poshy anatumia ARV (Dawa ya kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI) hatimaye jana, mwanadada huyo ameamua kuudhihirishia umma kuwa yeye yuko safi, na habari hizo ni uzushi tu na yenye lengo la kumchafua kwenye jamii baada ya kuamua kupima na kuweka majibu yake ya vipimo vya “ngoma” hadharani kwenye mtandao mmoja wa kijamii.
Katika picha hiyo mwanadada huyo aliandika kuwa ni vizuri kucheki afya yako mara kwa mara, picha iliyokuwa ikionesha kuwa majibu hayo ya ngoma yanaonesha kuwa mwandada huyo yuko HIV NEGATIVE.
Je wewe umepima? Majibu yanasemaje? Au ulikimbia majibu?
Majibu ya Amanda Kuhusu Madai ya Kutumia ARV
Staa wa Bongo Movies, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni aligeuka mbogo kwa shabiki wake aliyefahamika kwa jina la Joel baada ya kuambiwa eti ni mmoja wa wasanii wanaotumia vidonge vya ARV vya kuongeza siku za kuishi kwa waathirika wa Ukimwi.Ishu ilianzia kwenye mtandao wa Facebook ambapo Joel aliona picha ya Amanda akipima ugonjwa ambao haukujulikana ndipo kijana huyo alipokomenti kwamba eti msanii huyo ana ngoma.Akizungumza na Ijumaa, Amanda alisema amechoshwa na watu wanaomkashifu mtandaoni wakidhani kila msanii ni mhuni.
“Nimeona nimtolee uvivu kwani asifikirie Bongo Muvi wote tunatumia ARV, mimi nimepima mara ya mwisho juzi na najiamini najua ninachokifanya, alinikera sana yule kijana ndiyo maana nikampa makavu,” alisema Amanda.