Mwaka jana kuna tukio lililoshtua wengi duniani na kuzungumziwa sana kwenye vyombo vya habari kuhusu msichana Jolly Tumuhiirwe wa Uganda, aliyemfanyia ukatili mtoto wa bosi wake Arnellamwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kwa kumpiga vibaya baada ya kukataa kula chakula.
Wakati hilo halijasahaulika tukio linalokaribia kufanana na hilo limetokea tena Kenya.. msichana ambae anafanya kazi za ndani amekutwa akilazimisha kumnyonyesha mtoto wa bosi wake.
Msichana huyo Grace Mwikali Mwema amekutwa akifanya kitendo hicho siku mbili tangu aanze kazi japo jaribio lake halikufanikiwa kwa kuwa mtoto alikataa kunyonya.
Mama wa mtoto huyo amesema aligundua kitendo hicho kutokana na camera aliyoitega nyumbani kwake na akuunganisha na simu yake ya mkononi.
Msichana huyo anashikiliwa na Polisi akisubiri kupandishwa kizimbani.
Hii ni video ambayo inaonesha tukio lote…