Sunday, April 19, 2015

Picha za Uchi za Mume Wa Mtu Akiwa na Mchepuko Wake Zavuja na Kusambaa Mtandaoni


Kaloli  Dawa ambaye ni mume wa mtu, amedaiwa kujipiga picha za utupu akiwa na mchepuko wake uliofahamika kwa jina moja la Irene kisha kusambaa mitandaoni.
  
Picha za wawili hao wenyeji wa Wilaya ya Lamadi, mkoani Simiyu zimedaiwa kuvuja mara baada ya rafiki wa Irene kuziiba kwenye ‘laptop’ ya Kaloli na kuzisambaza mtandaoni.

Imedaiwa kuwa rafiki wa Irene ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alizivujisha picha hizo baada ya kugombana na Irene.
  
Imeelezwa kuwa, vijana hao ni watoto wa wafanyabiashara wakubwa hivyo kitendo cha kusambaa picha hizo kimewasononesha.
  
Mwanahabari wetu alimtafuta mzazi wa Kaloli, Mzee Kaloli kumsikia anazungumziaje tukio hilo.
  
“Ni kweli nimeziona hizo picha yaani ni aibu sana kwangu maana mimi ni mtu na heshima zangu na nimeshamkanya mara kadhaa mwanangu aachane na huyo Irene lakini hata hasikii.
  
“Asiyesikia la wazazi atafunzwa na ulimwengu nimeshaongea sana na Kaloli atulie na mkewe na hata huyo Irene mbona king’ang’anizi hivyo wakati mwanangu ana mke wake tena ana mtoto mdogo?  Wataniua kabla ya umri wangu nimechoka na tabia za Kaloli ananitia aibu,” alisema Mzee Kaloli.