Seleman Msindi aka Afande Selle anawania kuwa mbunge mtarajiwa wa jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi cha chama cha ACT Tanzania, na haogopi maneno ya ‘haters’ wanaotaka kukiwekea mchanga kitumbua chake kwa mambo yaliyopita.
Bila shaka unakumbuka ile picha ambayo Afande alipigwa akiwa amevua nguo na kubakia na boxer tu jukwaani wakati akitumbuiza!
Mfalme huyo wa Rhymes anaamini kuwa picha haiwezi kumchafulia CV yake mbele ya waajiri wake watarajiwa aka wananchi wa Morogoro Mjini.
“Hainiumizi, inanifurahisha,” Afande aliiambia 255 ya XXL, Clouds FM.
“Inanifanya nione kama namuenzi ipasavyo mfalme Daudi baba yake Suleiman. Inanifanya niamini kwamba ufalme wangu haukuwa wa kubebwa. Kwahiyo mpaka hapo inaashiria utashi wangu, hadhi yangu na ufalme wangu ambao leo hii unaenda kuwa ubunge wa Morogoro.”
Unadhani Afande anaweza kuwa mbunge mzuri wa Morogoro Mjini?