Thursday, May 21, 2015

Anti Lulu Awatishia Wake za Watu


Staa wa Bongo Movies na mtangazaji mwenye vituko vingi na kujiachia kwa sana amekuja na mpya nyingine ya kuwakanya wanaomtukana katika mitandao ya kijamii kila anapoweka picha zake.
 
 Anti Lulu amesema asilimia kubwa ya watu wanamtukana anapoweka picha zinazomuonesha maumbile yake  ni wanawake.
 
 
"Asilimia kubwa ya wanawake ndio wanaongoza kunitukana nikiweka picha zangu za Mungu alivyoniumba ..mapaja yangu,hips zangu ma**ko yangu...sasa sijui kwanini mwatukana nyie wanawake angalieni nisiwabebee mabwana au wanaume zenu kwa mlioolewa,mimi mmakonde na Mbondei..mtalia na kusaga meno" aliandika hivyo katika ukurasa wake wa facebook.