Tuesday, May 19, 2015

CHRIS BROWN, NICKI MINAJ VINARA WA KUTAJWA TUZO ZA BET 2015

Chris Brown na Nicki Minaj wote wanawania tuzo katika vipengele 6.
WANAMUZIKI Chris Brown na Nicki Minaj wameongoza kwa kutajwa mara nyingi katika vipengele vya kuwania Tuzo za BET 2015 kwa kila mmoja kutajwa mara sita.
Nicki Minaj.
Katika kipengele cha video bora ya mwaka, Brown ametajwa mara mbili kwa video zake za Loyal na New Flame.
Minaj naye yupo juu akitajwa katika vipengele sita kikiwemo cha video bora ya mwaka kwa wimbo wake wa Anaconda huku Beyonce na Lil Wayne wakifuatia kwa kutajwa katika vipengele vinne.
Brown pia ametajwa katika vipengele vya Mwanamuziki Bora wa Kiume wa R&B/Pop, Tuzo ya chaguo la watazamaji na akitajwa tena mara mbili katika vipengele vya Colabo bora kwa wimbo wake wa Loyal, aliomshirikisha Lil Wayne na Tyga, pamoja na wimbo wake wa New Flame, aliowashirikisha Usher na Rick Ross.
Chris Brown akiwa amembeba mwanaye.
Kwa upande wa Minaj yeye anawania pia katika vipengele vya Mwanamuziki Bora wa Kike wa Hip hop, Kundi Bora akiwa ni miongoni mwa wanamuziki wa Kundi la Young Money na Colabo Bora kwa kushirikishwa kwenye wimbo wa No Love akiwa na August Alsina.
Pia ametajwa mara mbili katika kipengele cha Tuzo ya chaguo la watazamaji kwa ngoma yake ya Only na kwenye ngoma ya Rae Sremmurd ya Throw Some Mo aliyoshirikishwa.
Beyonce.
Mwanamuziki Beyonce yeye yupo katika vipengele vya Mwanamuziki Bora wa Kike wa R&B/Pop, Video ya mwaka, Mwongozaji wa mwaka na Tuzo za chaguo la watazamaji.
Tuzo hizo zitatolewa Juni 28, mwaka huu nchini Marekani.