Cristiano Ronaldo ni zaidi ya mchezaji kama wachezaji wengine wanavyojaribu kujitolea kwenye mambo mbalimbali. Hivi karibuni lilitoka tetemeko la ardhi huko Nepal na kusababisha karibia watu 7000 kupoteza maisha.
Nchi hiyo imekua kwenye hali ya kuitaji msaada wa hali na mali na watu pamoja na nchi mbalimbali zimeshiriki kwenye kuchangia michango mbalimbali ili kusaidia watu walioathirika.
Zaidi yak u-tweet kuhusu janga hili, pia Ronaldo imeripotiwa ametoa pesa zake pound milioni 5 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko hili.Ronaldo zaidi ya kuwa mfanyabiashara na mchezaji, pia anatambulika kwa kuwa mtu ambae anajihusisha sana na maswala ya kijamii kama hivi.