Sunday, May 17, 2015

CRYSTAL PALACE WAVURUGA ‘SEND OFF’ YA GERARRD ANFIELD, WAIPIGA 3-1 LIVERPOOL

LIVERPOOL imefumuliwa mabao 3-2 na Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Anfield.
Matokeo hayo yanaifanya Liverpool ibaki na pointi zake 62 baada ya kucheza mechi 37, ikiwa nafasi ya tano nyuma ya mahasimu, Manchester United wenye pointi 68 za mechi 36.
Chelsea wenye pointi 84 za mechi 36, wapo kileleni na ndiyo mabingwa tayari, wakifuatiwa na Manchester City wenye pointi 73 zamechi 36, wakati Arsenal yenye pointi 70 za mechi 35 wapo nafasi ya tatu.
Adam Lallana alianza kuifungia Liverpool dakika ya 26 akitumia vizuri makosa ya safu ya ulinzi ya Crystal Palace.
Lakini Jason Puncheon akaisawazishia Palace dakika ya 43 kwa shuti la mpira wa adhabu, kabla ya Wilfried Zaha kufunga la pili dakika ya 60, zikiwa ni dakika 22 tangu aingie kutokea benchi. 
Zaha akapata penalti ya utata dakika za mwishoni, ambayo refa Jon Moss aliamua kimakosa kuiweka ndani ya boksi- na Glenn Murray akafunga bao la tatu dakika ya 90.
Nahodha Steven Gerrard alikuwa anacheza mechi yake ya mwisho Uwanja wa Anfield akiwa na Liverpool kabla ya kuhamia LA Galaxy ya Marekani.
Liverpool; Mignolet, Can, Skrtel, Lovren, Ibe/Lambert dk65, Gerrard, Henderson, Moreno/Sinclair dk87, Lallana, Sterling na Coutinho/Lucas dk65.
Crystal Palace; Hennessey, Ward, Kelly, Dann, Souare, Puncheon, McArthur, Ledley, Lee/Zaha dk59, Chamakh/Mutch dk76 na Bolasie/Murray dk83. 
Zaha tapped in amid calls for offside just 22 seconds after being brought off the bench by Alan Pardew 
Mshambuliaji Wilfried Zaha akishangilia baada ya kuifungia Crystal Palace katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Liverpoool leo