Sunday, May 17, 2015

WINGA MPYA WA MAN UNITED 'BISHOO' HUYOO, ATUA ENGLAND KWA DEGE LA KUKODI

WINGA wa kimataifa wa Uholanzi, Memphis Depay amewasili England kwa mara ya kwanza tangu akubalia kuhamia Manchester United kwa dau la Pauni Milioni 25.
Depay amewasili England kwa ndege ya kuposti picha yake akiwa kwenye ndege hiyo ikiwa imeambatana na maelezo; "Siku kubwa leo, naelekea England kwa viatu vipya vya mpira Under Armour,".
Mchezaji huyo mpya wa Manchester United awali aliposti picha yake akifurahia na wachezaji wenzake watatu wa PSV wakifurahia jua na kupata mlo wa asubuhi huko Ibiza Jumanne.
Mchezaji mpya wa Manchester United, Memphis Depay akiwa ameketi kwenye ndege ya kukodi kwa safari ya London