KLABU ya Manchester United itapambana na Arsenal kugombea saini ya kipa Petr Cech iwapo David de Gea atakataa kuongeza Mkataba mpya na kusaini Real Madrid.
Madrid imeamua kuongeza juhudi za kuwania saini ya De Gea arejee nyumbani Hispania, baada ya wiki iliyopita kutolewa katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Juventus. Na hiyo inatokana na kushuka mno kwa kiwango cha kipwa wake wa muda mrefu, Iker Casillas.
Kipa wa kimataifa wa Hispania, De Gea, ambaye alijiunga na Manchester United kwa Pauni Milioni 18 kutoka Atletico Madrid miaka minne iliyopita, amekuwa akihusishwa mno na kurejea nyumbani kwao kufanya kazi.
Petr Cech ameshinda mataji yote na Chelsea na sasa anatarajiwa kwenda kuchukua nafasi ya De Gea iwapo ataondoka Manchester United
David de Gea ni bidhaa adimu Ligi Kuu England, ambayo inatakiwa na Real Madrid
United imejaribu kumzuia kipa huyo kwa kumpa ofa ya mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki, ambayo itamfanya awe anayelipwa zaidi kihistoria katika soka.
Lakini inafahamika kwamba De Gea anaweza kukubali mshahara mdogo ili mradi tu ajiunge na Real.
Arsenal, Liverpool, Paris Saint-Germain na Besiktas nazo zote zinataka huduma ya Cech ambaye kwa sasa anasugua benchi Chelsea baada ya kurejea kwa kipa Mbelgiji, Thibaut Courtois msimu huu, na sasa United inaongezeka.