Najua watu wengi waliisubiri hii kwa hamu.. wengine hata sio mashabiki wa boxing lakini walijikuta wakivutiwa na hii.. Promo ilikuwa kubwa sana, pambano la kihistoria ambalo dunia nzima ililisubri ni hili kati ya Floyd ‘Money’ Mayweather na Manny Pacquiao.
Points tayari zimeamua, pambano limeenda kwa round 12, Floyd Mayweather kamshindaPacquiao kwa points sita tu.. Floyd ana points 117 na Pacquiao ana points 111.
Kwa matokeo hayo Mayweather kaendeleza kuweka rekodi yake kubwa ya kutoshindwa pambano hata moja tangu amekuwa professional boxer.
Shilingi yako uliweka upande upi mtu wangu ?? Nitafurahi kuona utakachoniandikia kuhusu hii..