Wednesday, May 20, 2015

HAYA NI MAMBO 10 AMBAYO UNAWEZA KUWA HUYAJUI KUHUSU LIONEL MESSI

messi messi
1.Kuzaliwa na familia yake
Lionel Messia amezaliwa June 24 huko Rosario Argentina sehemu moja aliyozaliwa Che Guevera na familia yao ina uasili wa Italy. Baba yake alifanya kazi kama mfua vyuma lakini pia mpira  haujaanzia kwa Messi tu, baba yake alikua kocha wa timu ya mtaani.
2.Utotoni
Kama watoto wengine hasa hasa wavulana wamekulia kimtaa mtaa. Lakini Messi alikua na matatizo ya kuumwa na matibabu yake akiwa na miaka 11 yalikua ni $900 kwa mwezi ambayo familia yake ilikua haina uwezo huo.
3.Mkataba wake
Baada ya Sporting director Carles Rexach kuwa impressed na kiwango cha Messi akiwa na miaka 13. Alimsainisha mkataba Messi kwenye Napkin paper baada ya kutopatikana karatasi official kwa wakati ule. Tangu hapo Barcelona ilikua ina gharamia matibabu ya ugonjwa wa Messi
4.Akiwa Barcelona
Kwa mara ya kwanza anacheza mechi na Barcelona alikua na miaka 17 dhidi ya RCD ESpanyol na akiwa mchezaji namba tatu mwenye umri mdogo kuwai kuchezea Barcelona. Pia akaweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo kuwai kuifungia Barca.
5.Mafanikio
Messi amewai kushinda medali ya dhahabu mwaka 2008 huko Beijing akiwa na timu ya Argentina. Ameshunda La liga,Copa  Del Rey,Super cup,Uefa,Uefa Super Cups na Club World Cups.
Ameshinda FIFA Ballon d’Or rekodi ya mara 4 mwaka 2009,2010,2011 na 2012.Pia ameshinda kiatu cha dhahabu cha ulaya mara 3
6.Majukumu ya kijamii
Messi ni balozi wa UNICEF kwa muda mrefu sana,Messi pia mwaka 2013 aliwai kutoa msaada wa $812,000 kwa ajili ya kujenga hospitali za watoto huko kwao Rosario.Pia aliwai kuwalipia madaktari kwenda Barcelona kwa ajili ya kupata mafunzo zaidi ya udaktari wa watoto
7.Kufananishwa na legend
Mara nyingi Messi ametajwa kuwa ni mrithi wa Maradona na Maradona ameshasema kwamba anakubali kuwa huyu ni mrithi wake. Japokua Maradona hajawai kushinda tuzo ya FIFA Player of the year na Messi ameshashinda. Wengi wanasema tuzo hiyo imelewa muda ambao Maradona yupo kwenye mwisho wa kiwango chake.
8.Familia
Messi amemuoa Antonella Roccuzzo na wana motto mmoja anaitwa Thiago amezaliwa November 2, 2012. Messi ana tatoo ya mtoto wake mguuni na pia anategemea kupata mtoto mwingine
9.Kuwa na aibu
Messi ni mtu wa aibu tangu yupo mtoto, Tabia hiyo imeendelea hadi ukubwani, Mara chache sana anaongea na hata kuongea na simu ni mara chache sana. Ujumbe wa muhimu kwenda kwa Messi huwa unatumwa kwa SMS.
10.Style ya kushangilia
Mara nyingi anaonekana akishangilia kwa kuonyoosha vidole juu. Hiyo ni ishara yake kwamba anamamini bibi yaake yupo juu anamuangalia akicheza mpira. Messi alimpoteza bibi yake akiwa na miaka 10.