Monday, May 11, 2015

KUMBE! ZARI, MADAM RITA NI NDUGU

Musa Mateja na Gabriel Ng’osha
Kumbe! Machoni pa wengi maswali yaliibuka miongoni mwa mashabiki wa mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’ baada ya kumuona akiwa ‘klozi’ na Bosi wa Bongo Stars Search (BSS), Rita Paulsen ‘Madam’ kwenye shoo ya Zari All White Party iliyofanyika juzikati kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar.
Madam Rita akiwa katika pozi na Zari walipokua kwenye Zari All White Party.
Katika ‘iventi’ hiyo, Madam Rita alikuwa beneti na Zari hivyo baadhi ya watu walikwenda mbali zaidi na kudhani labda Madam alikuwa kama bodigadi’ wa Zari ili kusaidia linapokuja suala la kumwaga ung’eng’e a.k.a kutema yai lakini Ijumaa Wikienda limefanya kazi yake na kubaini kwamba wawili hao ni ndugu kabisa.
Wakiwa katika pozi.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba Zari na Madam Rita si ndugu wa tumbo moja ila mama zao ndiyo wenye undugu wa damu kwani wanaitana binamu.
Ilifahamika kwamba, Zari amekuwa akikutana na Madam Rita mara kwa mara anapokuwa Bongo, ikiwa ni pamoja na kushauriana mambo kibao ya kimaendeleo hasa katika suala zima la kuona fursa kwenye ishu za burudani.
Madam Rita, Diamond na Zari wakiwa katika picha ya pamoja.
Imebainika kuwa ukiachana na kukutana Bongo, ndugu hao wamekuwa wakikutana Sauzi kwenye mishemishe zao za kusaka ‘mahela’.
Kwa mujibu wa Madam Rita, mbali na undugu, anamkubali Zari katika pilikapilika za kusaka maisha lakini pia Zari naye anamkubali Madam Rita kwa harakati zake za utafutaji na kupambana na umaskini.
“Zari ni mwanamke mtafutaji na ni ndugu yangu kabisa. Unajua pale Mlimani City watu walikuwa wanauliza tupoje, wengine walidhani nipo na AKA (msanii wa Afrika Kusini) lakini ukweli ni kwamba mimi na Zari tunafahamiana vizuri,” alisema Madam Rita.