Monday, May 11, 2015

MAMA AIBIWA MTOTO KLINIKI..ACHEZEWA MCHEZO WA KIMAFIA SANA

Inauma sana! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Martha Masawe (20), mkazi wa Kilakala mkoani hapa, ameibiwa mtoto mchanga mwenye umri wa siku 34 akiwa katika Hospitali ya Nunge, Ijumaa Wikienda lina ‘full’ stori.
Martha Masawe akiwa kwenye foleni.
Tukio lililofanywa kimafia lilijiri Ijumaa iliyopita saa 7:00 mchana wakati Martha akiwa kwenye foleni.
Akihojiwa na Ijumaa Wikienda huku akiangua kilio hospitalini hapo Martha alisema:
Martha Masawe akilia kwa uchungu baada ya kuibiwa mwanae.
“Usiku wa kuamkia leo (Ijumaa) mwanagu alikohoa sana, asubuhi baba yake aliniambia nimlete hospitali kucheki kifua.
“Nikiwa kwenye foleni alikuja mama mmoja, akaomba amshike mwanangu huku akisema ni mzuri.
“Baadaye aliniuliza ana tatizo gani? Nikamwambia anaumwa kifua, akanishauri twende dukani tukamnunulie sweta.
“Tulikwenda maduka ya Kikundi tukanunua sweta na nguo nyingine kisha kila mtu akapanda bodaboda yake tukaanza safari ya kurudi hospitali.
Martha Masawe akiwa hajui afanye nini baada ya kuibiwa mwanae.
“Chaajabu nafika hapa hospitali nimekaa zaidi ya nusu saa yule mama hajatokea. Nikawasimulia manesi wakadai tayari nimeibiwa mtoto.”
Baadaye mama huyo alipata msaada wa askari wa doria, afande Mwajabu aliyeongozana naye kwenda kituo cha polisi kufungua mashtaka na namna ya kumuelewesha mumewe.