Majukumu! Mkongwe wa sinema za Kibongo ambaye amekita makazi yake nchini Denmark, Lucy Komba ameweka bayana kuwa katika suala la mapishi anapokuwa nyumbani, huwa wanawekeana zamu ya kupika na mumewe.
Lucy alivujisha taarifa hiyo baada ya mwanahabari wetu kumuuliza juu ya ratiba zake za mapishi anapokuwa nyumbani ndipo alifunguka:
“Huwa tunawekeana zamu ya kupika na mume wangu, mfano kama leo, mimi nipo nyumbani lakini sipiki namsubiri atoke kwenye mihangaiko yake aje apike, huku ndivyo mambo yanavyokwenda tofauti kidogo na huko nyumbani (Bongo) kwamba mwanamke pekee ndiye mwenye jukumu la kupika.”