Friday, May 22, 2015

MABIFU YA WEMA YAMCHEFUA SHAMSA

Na Imelda Mtema
 Kitendo cha Wema Sepetu kugombana mara kwa mara na kila mtu anayekuwa rafiki yake, kimeonesha kumkera staa mwezake Shamsa Ford ambaye anasema alipofikia watu wataogopa kujenga ushosti naye.
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford.
Akizungumza na mwandishi wetu, Shamsa alisema ni kweli watu kugombana ni kitu cha kawaida lakini kwa Wema anatakiwa ajiangalie upya ili watu wasimfikirie vibaya. “Kwa kweli sifurahishwi na hii hali ya Wema kugombana na kila rafiki yake, mwishowe tutaogopa sasa kujiweka karibu naye,” alisema Shamsa.
Wema Sepetu.