MVUA zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar, sasa imegeuka kuwa majanga kwa kusababisha mafuriko ambayo yamekwamisha shughuli nzima kwa wananchi waishio katika jiji hilo kufuatia barabara nyingi kutopitika kwa urahisi.
Kamera yetu leo asubuhi imefanikiwa kutembelea baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar na kukuta yakiwa na mafuriko kutokana na mvua hizo zinazoendelea kunyesha.