Friday, May 29, 2015

MAYWEATHER 'MTU PESA' APIGA MILIONI 400 NJE YA ULINGO

BONDIA Floyd Mayweather amesherehekea kuingiza fedha nyingine, baada ya kushinda dola za Kimarekani 200,000 (Sh. Milioni 400) katika mechi ya mpira wa kikapu kwa kupanda ndege yake binafsi kwenda Seattle.
Mayweather maarufu kama 'Mtu Pesa' kwa jina la utanialiweka dau la dola 200,000 katika mechi ya Golden State Warriors dhidi ya Houston Rockets, mechi ya tatu ya Fainali za Kanda ya Magharibi.
Bingwa wa dunia asiyepingika alipata mara mbili Jumapili usiku baada ya Warriors kuifunga Rockets 115-80 kwenye mechi hiyo.
Bondia huyo amekuwa na bahati ya kushinda mara kwa mara kila anapoweka dau, iwe kwenye ndondi au mpira wa kikapu. Lakini pia ndiye bondia anayeongoza kulipwa duniani akiwa pia mwanamichezo tajiri zaidi duniani.
Floyd Mayweather celebrated his $200,000 betting win by jetting off to Seattle with distant cousin Dejuan Blake
Floyd Mayweather akisherehekea dola 200,000 alizoshinda kwa kupanda ndege yake binafasi kwenda Seattle na mpwa wake, Dejuan Blake
Mayweather doubled his money after placing $200,000 on the Golden State Warriors match on Sunday night
Mayweather amepata mara mbili ya dau aliloweka, dola 200,000 kuitabiria ushindi Golden State Warriors Jumapili usiku