Friday, May 22, 2015

MOURINHO, HAZARD WATWAA TUZO ENGLAND

Jose Mourinho.
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho ametwaa tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu ya England kwa msimu huu wa 2014/2015 huku mchezaji wake Eden Hazard akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu.
Eden Hazard.
Hazard amechukua tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu yake kutwaa taji la Ligi Kuu ya England huku akiifungia mabao 14.
Hazard alikuwa akiwania tuzo hiyo pamoja na wachezaji wengine saba ambao ni: John Terry, Cesc Fabregas, Nemanja Matic, Sergio Aguero, David de Gea, Harry Kane na Alexis Sanchez.