Bondia Pacquiao amerejia nchini kwake Ufilipino baada ya kufanyiwa upasuaji wa bega huko Marekani.
Pamoja na bondia huyo nyota wa dunia kushindwa baada ya kupigwa na mwenzake Floyd Mayweather raia wa nchi hiyo walionyesha kuendelea kumwamini na kujitokeza kwa wingi kumpokea.
Pacquiao alionekana muda wote akiwa na furaha licha ya maumivu ya upasuaji wa bega pamoja na kutofanya kile alichokidhamiria katika pambano hilo lililoweka historia duniani lililofanyika May 2, Las Vegas, Marekani
Pacquiao alipigwa kwa pointi na mpinzani wake na mara baada ya pambano kuliibuka lawama kuhusu bondia huyo kucheza huku akiwa mgonjwa