Noma sana! Kijana mmoja ‘sharobaro’ ambaye jina halikufahamika amenusurika kufanyiwa kitu mbaya ‘kubonyezwa kizenji’ na wahuni baada ya kupiga mitungi na kuwa chakari.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati ambapo jamaa huyo alikutwa kwenye kichaka maeneo ya Holowela, Mji Mpya mkoani hapa huku suruali ikiwa magotini.
“Tulikuwa tunatoka kwenye kigodoro mishale ya saa 7:00 usiku.
“Tulipofika hapa tumemkuta huyu jamaa akiwa kwenye hiki kichaka akionekana kulewa.
“Baada ya kumchunguza tumeshindwa kumtambua kwani siyo mkazi wa mtaa huu hivyo wahuni wanaweza kumfanyia chochote,” alisema mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Madodo.