Thursday, May 28, 2015

RAY, CHUCHU HANS WAONESHANA MAHABA HADHARANI!

Richard Bukos
MAHABA popote! Licha ya kudaiwa ‘wamemwagana’, wapenzi wawili ambao ni wasanii ndani ya Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans wameoneshana mahaba mazito hadharani na kuwaziba midomo waliodhani hawawezi kuwa pamoja tena.
Wasanii ndani ya Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans wakionyeshana mahaba.
Ishu hiyo ilinaswa hivi karibuni na ‘kasuku’ wetu maeneo ya Posta jijini Dar, kulikokuwa na sherehe za utoaji wa tuzo za filamu (TAFA) na kuwafanya watu wengi kushangaa huku wakionekana kuteta kwa nyakati tofauti.
“Mmh, hawa wamerudiana kwa mahaba mazito namna hiyo tena? Mbona tulisikia wameachana sasa naona wamegandana tena,” alisikika msanii mwingine (jina tunalo).
Hata hivyo, mwandishi wetu alimfuata Ray na kumuuliza kuhusu minong’ono ya wao ‘kutemana’ ambapo alijibu;
 “Huyu ndiye mke wangu, hayo mengine achana nayo kabisa.”