Thursday, May 28, 2015

JUMA NATURE ATOA MSAADA HOSPITALI YA MBAGALA

Muuguzi akijaribu kumpatia maelekezo ya wagonjwa wa hospitali hiyo baada ya mgonjwa kuingizwa katika wodi.
Mmoja wa watu walioambatana na Juma Nature akifungua boksi lenye mashuka katika hospitali ya Mbagala.
Mdhamini wa hafla hiyo, Mansoor Y.Kipolelo (kushoto mwenye tai) akitoa ufafanuzi kabla ya kutolewa zawadi hizo.
Juma Nature akikabidhi msaada wa mashuka (kushoto) kwa katibu wa afya hospitali ya Mbagala (kulia). Wanaoshuhudia pembeni kulia ni wauguzi wa hospitali hiyo.
Nature pamoja na katibu wa afya wa hospitali ya Mbagala waliyeshikana mkono akimkabidhi chandarua huku akishuhudiwa na watu mbalimbali waliokuwepo.
Juma Nature (wa pili kulia) akiondoka hospitalini hapo baada ya kukabidhi zawadi.
MKONGWE katika muziki wa Bongo Fleva, Juma Kassim Ally ‘Nature’ ametoa msaada wa mashuka na vyandarua katika Hospitali ya Mbagala- Zakhem jijini Dar kama ishara mojawapo ya kuadhimisha miaka 16 tangu aanze muziki.
Staa huyo alitoa zawadi hizo leo ambapo alikuwa ameambatana na baadhi ya wasanii pamoja na mdhamini wa sherehe hiyo, Mansoor Y.Kipolelo na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kurasini, Mjimpeye.
Kabla ya kutoa zawadi hizo, Nature aliwatembelea wagonjwa waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo na kuwafariji huku akimwomba Mungu kuwaponya haraka na kurudi katika hali yao ya kawaida.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu wa Afya wa Hospitali, Edwin P.Bisakala baada ya kukabidhiwa msaada huo alisema kuwa amefurahishwa sana jinsi msanii huyo wa muziki wa Bongo Fleva, Juma Nature alivyoguswa na wagonjwa hadi kulazimika kwenda kutoa zawadi ya mashuka, vyandarua pamoja na maji ya kunywa kwa wagonjwa, kama mojawapo ya kusherehekea miaka 16 ya kuwa katika muziki hivyo kuwataka wasanii wengine kuiga mfano wake.
“Nimefurahishwa sana kwa kitendo cha Juma Nature kukumbuka hospitali hii kwa kutuletea mashuka, vyandarua pamoja na maji ya kunywa kwa wagonjwa wetu hivyo nawaomba  wasanii wengine waige mfano wake,” alisema Bisakala.
Aidha ametoa wito kwa wadau na mashabiki wote kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha hilo ambapo kutakuwa na wasanii mbalimbali watakaotoa burudani siku hiyo.
Sherehe hizo za kutimiza miaka 16 zinatarajiwa kuambatana na kutimiza kwa mwaka mmoja kwa kituo cha redio cha 93.7  EFM keshokutwa kuanzia jioni katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, Mei 30, Mwaka huu huku kiingilio kikiwa ni shilingi 7,000 tu.