Tuesday, May 12, 2015

TYGA AANZA KUFIKIRI NDOA NA KYLIE

Mwanamuzuki wa miondoko ya kufoka, Tyga.
Los Angeles, Marekani
MSANII wa miondoko ya kufoka, Tyga, 25, amesema baada ya kuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu na mpenzi wake ambaye ni mdogo wa mwanamitindo, Kim Kardashian, Kylie Jenner, 17, sasa wana mpango wa kuishi kama mke na mume.
Tyga akiwa na mpenzi wake Kylie Jenner.
Chanzo cha karibu na mastaa hao kilisema Tyga ana mpango wa kumuoa Kylie Jenner, 17, ili aishi naye pia wamtoe nishai aliyekuwa mpenzi wake, mwanadada Blac Chyna, 26, ambaye alizaa naye mtoto mmoja anayefahamika kwa jina la King Cairo Stevenson, Blac amekuwa akiuonea gele uhusiano huo.
Katika kuonyesha mapenzi yake kwa Kylie, Tyga amechora jina la mpenzi wake huyo mkononi akiashiria kuwa amezama.“Tyga ana mapenzi ya dhati na Kylie. Ana mpango wa kuishi naye pindi muda ukiwa tayari. Unajua anapenda sana kuishi na Kylie maisha yake yote,” kilisema chanzo.
Kylie anatarajiwa kufikisha miaka 18, Agosti mwaka huu hivyo utakuwa muda muafaka wa  yeye kuanzisha familia na Tyga.