Friday, May 22, 2015

WANAFUNZI UDOM WAGOMA WAKIDAI PESA ZAO ZA MIKOPO KWA AJILI YA KUJIKIMU

Wnafunzi wa UDOM wakiwa katika mgomo wakishinikiza serikali kuwalipa pesa zao za kujikimu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa akiwatuliza na wanachuo.
Wakiwasikiliza Naibu Waziri wa Afya Steven Kebwe na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa.
Siku ya pili ya mgomo huo.
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha UDOMA, Mkoani Dodoma wameamua kuacha masomoyao tangu jana na kugoma wakishinikiza Bodi ya Mikopo kulipa pesa zao za mikopo kwa ajili ya kujikimu.
Mgomo huo unakuja siku mbili tu baada ya wenzao wa UDSM, Dar es Salaam kugoma kwa madai kama hayo na hatimaye siku iliyofuatia wakalipwa pesa zao.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alilazimika kumtuma Naibu Waziri wa Afya Steven Kebwe na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa ili kuwatuliza wanafunzi hao waliokuwa wakidai kuishi katika mazingira magumu baada ya kukoswa pesa za kujikimu na kufanya kushindwa kufuatilia masomo yao.
Hali hiyo ilionekana kama kutulia kwa muda, lakini leo yameibuka mapya baada ya wanafunzi haokugoma tena wakiendelea kudai pesa zao za mkopo.
Akizungumza na mwandishi wetu, mwanafunzi mmoja wa UDOM (kwa sharti la kutotajwa jina lake kutajwa) alisema kuwa, "asubuhi ya leo tumegoma kuingia madarasani tukidai haki yetu, pesa zetu za mkopo hatujapata, tunaishi katika mazingira magumu. Maisha ya hapa chuo yamekuwa magumu sana, kwa mfano mimi nimekopa pesa kama laki moja mpaka sasa tangu hali hii ya kukoswa 'boom' ianze lakini bado maisha yamekuwa magumu kwa upande wetu. Tunalazimika kula mara moja kwa siku. Tunaomba serikali isikilize kilio chetu tunapata shida sana, tuanshindwa kufuatilia masomo yetu kwa kutumia muda mwingi kuwaza tutakula nini, tutaishi vipi na mpaka lini kwa hii hali."
Taarifa zinaongeza pia kuwa wamepigwa mabomu ya machozi na Jeshi la Polisi likiwataka kutawanyiaka eneo walilokuwa wamekusanyika. Kikosi cha kuzuia ghasia maarufu kama FFU wamezingira eneo lote la chuo na wanafunzi wapo mabwenini.