Wednesday, June 24, 2015

ALI KIBA ATIMULIWA KWENYE NYUMBA

Ali-KibaNyota wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba.
Waandishi Wetu
LICHA ya mwenyewe kukanusha vikali lakini madai mazito yanasema kuwa, nyota wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ametimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi iliyopo Kunduchi-Beach jijini Dar baada ya kukosana na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake ambaye pia ndiye mmiliki wa mjengo huo.
Habari kutoka kwa chanzo makini zinaeleza kuwa, pamoja na Kiba kuendelea kusisitiza kwamba si kweli, mwanamke huyo anayeishi nchini Singapore, aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kusoma kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari kuwa, kwa sasa Kiba anatoka na Miss Tanzania namba 2, 2006, Jokate Mwegelo ëKidotií huku Kiba mwenyewe akikataa madai hayo.
ajimet72Mjengo ambao Ali Kiba anadaiwa kutimuliwa .
KISIKIE CHANZO
Hivi jamani! Mnajua kuwa, Ali (Kiba) ametimuliwa kule Kunduchi-Beach kwenye ile nyumba aliyowekwa na yule demu mwenye fedha zake na ndiye aliyekuwa akimgharamia kila kitu?
Aliyemponza ni yule Kidoti, Jokate Mwegelo. Jokate amekuwa akimposti Kiba kwenye mitandao ya kijamii, ndipo mwanadada huyo alipoona akachukia na kumuona Kiba ameshindwa kuthamini fadhila zake, kilidai chanzo hicho makini.
ALI KIBA ATIMULIWA KWENYE NYUMBA (2)Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
ARUDI KWAO
Sasa hivi amerudi kwa mama yake, Kariakoo (Dar) kutokana na yeye mwenyewe kulikoroga kwa kuupiga teke mgodi wa fedha. Japokuwa mara kwa mara Kiba mwenyewe amekuwa akikanusha kujihusisha kimapenzi na Jokate, lakini ukweli ni kwamba ameshaharibu kwa mwanadada aliyekuwa anamuwezesha,î kiliongeza chanzo hicho.
ALICHOKISEMA MTU WA KARIBU NA KIBA
Baada ya kuvujishiwa nyeti hiyo, mapaparazi wetu walimtafuta mtu mmoja ambaye yupo karibu sana na Mbongo-Fleva huyo ambaye hakutaka jina lichorwe gazetini na kukiri kuwa, msanii huyo amehama Kunduchi-Beach, badala yake amehamia mjini kwa muda katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Ni kweli mshkaji (Kiba) sasa hivi haishi Kunduchi (Beach). Amehamia mjini (hakutaka kusema mjini ipi) ambapo anakaa kwa kipindi kifupi tu kisha atahamia kwenye makazi yake mapya maeneo ya Upanga (Dar) ambako kunafanyiwa ukarabati, alisema mtu huyo.
ALI KIBA SASA
Katika kuweka sawa mzani wa madai hayo, juzi mapaparazi wetu walimtafuta staa huyo wa Ngoma ya Chekecha Cheketua kwa njia ya simu na kumuuliza kuhusu madai hayo na kutaka kujua anakoishi hivi sasa, ambapo alifunguka hivi:
Unataka kujua naishi wapi ili iweje? Wakati unajua kabisa kuna matatizo yalinipata (kuvamiwa). Sasa nikisema si naweza kujitafutia matatizo mengine?
Siwezi kusema ninapoishi kwa usalama wa maisha yangu na kuhusu huyo mwanamke ni maneno ya watu wenye lengo la kunichafua.
AMZUNGUMZIA JOKATE
Jokate ni mwanamke ambaye nipo naye karibu katika vitu vingine ambavyo ni vya msingi zaidi na si hivyo ambavyo watu wanahisi. Lakini kama kuna mtu atahisi tofauti itakuwa juu yake. Mimi na Jokate ni washkaji ‘long time’ (muda mrefu) katika mambo kibao.
KUHUSU KUTIMULIWA KWENYE NYUMBA
Kuhusu nyumba nilishawahi kufafanua kwamba siyo yangu. Kuna mtu aliniweka kwa makubaliano maalum, lakini ninashangaa kusikia taarifa ambazo zipo tofauti juu ya ukweli ambao mimi ninaufahamu.
TUJIKUMBUSHE
Miezi kadhaa iliyopita kuliibuka utata juu ya umiliki wa nyumba hiyo baada ya kudaiwa ni ya Kiba lakini uchunguzi wetu ukabaini siyo yake, naye akakiri akidai kwamba alipanga.