Wednesday, June 24, 2015

Joto kali lawaua watu 700 Pakistan

Waziri mkuu nchini Pakistan Nawaz Sharrif ametaka hatua za dharura kuchukuliwa huku idadi ya watu waliofariki kutokana na wimbi la joto katika mkoa wa kusini wa Sindh ikifikia 700.

Mamlaka ya kukabiliana na majanga ya dharura NDMA imesema kuwa imepokea maagizo kutoka kwa Nawaz Sharrif kuchukua hatua za dharura.


 Jeshi tayari limepelekwa katika eneo hilo kujenga vituo vya kukabiliana na joto hilo ili kuisaidia mamlaka hiyo.

Wengi wa waathiriwa ni watu wazima kutoka kwa familia zinazopata mapato ya chini.


 Maafisa wa afya wanasema vifo vingi vimetokea katika mji mkuu wa Karachi ambao ulikumbwa na joto la viwango vya juu vya hadi digree 45 c.

Katibu wa afya katika mkoa wa Sindh Saeed Mangnejo amesema kuwa watu 612 walifariki katika hospitali kuu ya serikali mji huo katika kipindi cha siku nne zilizopita.



Wengine 80 wameripotiwa kufariki katika hospitali za kibinafsi.