Friday, June 26, 2015

BANZA STONE: MNANIUA SANA JAMANI!

Mwanamuziki nguli wa dansi, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’. Gladness Mallya

BAADA ya uvumi kuzagaa mtaani kwamba mwanamuziki wa dansi, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefariki dunia, Banza amesema amechoshwa na watu kumuua sana.
Baada ya uvumi huo, ndugu zake wamesema watu waache kumuua kwa maneno kwani bado yupo hai.
Ndugu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Hamis, alisema uzushi wa kifo cha Banza umewasumbua sana kwani watu mbalimbali walikuwa wakipiga simu na wengine kufika nyumbani jambo ambalo lilimuumiza sana Banza japokuwa anaumwa lakini akawa analalamika kwa nini watu wanamuua kwa maneno na si mara moja kutokea.
“Jamani yupo hai japokuwa anaumwa lakini anaongea tatizo lipo kwenye kusimama na kula, watu waache uzushi kwani wanamuumiza zaidi kwa uzushi wao huo,” alisema Hamis.