Wednesday, June 10, 2015

Cristiano Ronaldo acheza filamu inayoonesha mpaka uhasimu wake na Lionel Messi

CHELE9SWoAAym0O
FILAMU inayoelezea maisha ya nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronadlo kwa mwaka uliopita inatarajia kutoka baadaye mwaka huu.
Watengenezaji wa filamu hiyo wamesema Ronaldo ndiye mhusika mkuu na wanaamini itawavutia watu wengi kwani imeeleza vitu vingi kuhusu maisha ya mchezaji huyo bora wa dunia.
Filamu hiyo inatarajia kuonesha wapi alipanda na kushuka katika maisha yake ya soka mwaka uliopita na mpaka kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia, FIFA Ballon d’Or kwa mara ya tatu mwezi Januari mwaka huu.
Pia Filamu hiyo inatarajia kuonesha upinzani mkubwa kati ya Mreno huyo mwenye miaka 30 na nyota wa Barcelona, Lionel Messi.
Wakati Ronaldo anatoka kapa msimu huu wa La Liga, Lionel Messi ameiwezesha Barcelona kuchukua makombe matatu kwa maana ya La Liga, Copa del Rey na Uefa Champions League.
Jina la Filamu hiyo litatoa jibu kwa mashabiki wengi wa soka duniani ambao wamegawanyika juu ya nani ni mchezaji bora wa dunia kati ya Ronaldo na Messi.
Tayari Ronaldo amethibitisha kuwepo kwa filamu hiyo;
I’m happy to confirm that there’s a film being produced about me. Stay tuned for more info at @RonaldoFilm