Wednesday, June 10, 2015

MLELA: NIMEPATA MTOTO KWA BAHATI MBAYA!

YUSUF Godfrey Willard Mlela, muigizaji nyota wa filamu Bongo, alipata mtoto kwa bahati mbaya baada ya ‘kuuza mechi’ kwa msichana ambaye hakuwa na malengo naye kimaisha, lakini amelazimika kumhudumia kijana wake kwa kila kitu muhimu. 
muigizaji nyota wa filamu Bongo, Yusuph Godfrey Willard Mlela.
 Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, alisema alikutana na msichana huyo ambaye alikataa kumtaja jina kama rafiki wa kawaida, lakini akajikuta akishiriki naye bila kinga na siku hiyo hiyo akapata ujauzito ambao pia alishindwa kumshinikiza kuutoa kwa vile anatambua ni kitu kibaya.
 “Ilikuwa ni bahati mbaya, unajua mwanamke wa kumuoa ni yule ambaye mnazungumza na kupanga baada ya kujuana vizuri tabia.