Wednesday, June 10, 2015

SLIM AANGUA KILIO GARI LIKIENDA KWA MTALAKA

MUIGIZAJI mahiri wa filamu, Slim Mbegu ‘Slim’ hivi karibuni aliangua kilio akiwa Mahakama ya Mwanzo Magomeni baada ya kushuhudia gari alilopewa zawadi yeye na mkewe aliyetengana naye, Asia Morgana likivutwa kwa Break Down kusogezwa eneo hilo. 
Muigizaji mahiri wa filamu, Slim Mbegu ‘Slim’.
 Wawili hao walikuwa na shauri mahakamani hapo wakigombea gari hilo kila mmoja akidai ni mali yake halali, lakini hatimaye mwanamke alishindwa na hivyo Slim kuamriwa kulipeleka kortini ili liweze kukabidhiwa kwa wenyewe, lakini akashindwa kwa kushindwa kulifanyia matengenezo madogomadogo ya kulifanya litembee.
 Gazeti hili liliongea na Asia aliyemshukuru Mungu kwa kuweza kupata gari lake alilodai kusumbuliwa kwa muda mrefu na aliyekuwa mumewe, wakati Slim alisema hana la kusema zaidi ya kumuachia Mungu kila kitu.