Tuesday, June 16, 2015
EXCLUSIVE: FLORA MBASHA AWEKA WAZI KAULI YA MUMEWE
Staa wa nyimbo za injili hapa Taznania maarufu kwa jina la Flora Mbasha ambaye siku za hivi karibuni alichafua kurasa za mbele za magazeti kufuatia mgogoro wake na mumewe, Emanuel Mbasha ambaye aliangukiwa na tuhuma ya ubakaji, this is an exclusive issue kutoka kwa msanii huyo ambeye kwa sasa yupo nyumbani kwao Mwanza.
Akibonga na mwandishi wetu Flora alifunguka haya kuhusiana na hatua waliyo fikia yeye na mumewe hususani katika sakata la mgogoro wao.
“Namshukuru Mungu maana pamoja na kupitia katika kipindi kigumu lakini still bado ananipigania kila siku mashabiki wangu walizidi kunisapoti katika kipindi kigumu cha maisha nilicho kuwanacho.
Pia matatizo hayo hayakunifanya mimi kushindwa kumtumikia Mungu kwa kuimba muziki wa injili kwani najua yeye ndiye aliyenipa hiki kipaji na si mwanadamu, na uonapo mti unapigwa mawe sana jua kuwa ndiyo wenye matund amazuri
Hivyo basi Mumewangu nimemsamehe kwa moyo wangu wote wala sina hika ndani yangu, maana najua ni shetani tu aliyemtumikisha kufanya yote hayo.
Kauli ya mwisho na mumewangu aliniambia kuwa kama Familia yangu hawatamfutia kesi inayo mkabili mahakamani, basi atahakikisha sifanyi tena muziki hapa Tanzania na atahakikisha na hama nchi labda siyo yeye, maana atanichafua kwa Gharama zozote,so alinitishia kwa maneno hayo.
Kwa sasa washauri ni wengi inga si kila shauri nalichukua huwa naangalia yaliyo mema nachukua,
Kwa hayo yoye nawapenda sana watanzania wenzangu sasa na wote mnao sapoti kazi zangu sasa hivi namalizia kutengeza kazi yangu mpya, vile vile naangalia Promotor gani atanifaa kufanya nae kazi coz wengine ni matapeli tu maana kuna watuwengi wanataka kufanya kazi na mimi so lazima niangalie mtu mzuri.
Kazi yangu mpya itatoka soon so fans wangu wategemee utofauti mkubwa sana katika kazi hiyo coz inaujumbe wenye umguso kubwa sana ndani yake.
Mbali na hayo sasa hivi namuomba Mungu anisaidie nipate mtu wa kunidhamini ili nianze kuimba muziki wa live coz ni gharama kubwa, naamini kuwa naweza kuimba live na ninajiamini ila sija pata mtu wa kunisimamia” aliongeza .”sijui but Only God know ni lini tutaanza kuishi pamoja kama ivyo kuwa awali” Alisema Flora Mbasha