Tuesday, June 16, 2015

MMAJABU:TAJIRI AKUTA MAAJABU NDANI YA BARI!

Na Makongoro Oging’
MAAJABU! Tajiri mmoja mkazi wa jijini Dar es Salaam, Walter Urio anayemiliki biashara mbalimbali zikiwemo hoteli na baa, wiki iliyopita alikuta maajabu ndani ya gari lake baada ya mtu kuingia ndani wakati milango na madirisha yote yalikuwa yamefungwa, Uwazi linathibitisha.
Walter Urio meneja wa hoteli.
Tukio hilo la aina yake lilitokea nje ya Hoteli ya Nexus iliyopo Makumbusho karibu na kituo cha mabasi ambapo mtu huyo, Shaban Alphan alipopekuliwa, alikutwa akiwa na vitu vya ajabu kama ngozi ya fisi, tunguri na hirizi
Mwandishi wa gazeti hili aliyefika eneo la tukio mapema, alishuhudia umati mkubwa wa watu wakiwa wamelizunguka gari hilo aina ya Toyota Rav 4 lenye namba za usajili T732 BQV, wakimlazimisha kushuka ili wampe kipigo, wakimtuhumu huenda ni mshirikina aliyetumwa kummaliza tajiri huyo.
Kijana aliyekutwa kwenye gari.
Alipoulizwa sababu za kuingia katika gari hilo, Shaban alidai kuwa alipanda akiamini ni basi la abiria lifanyalo safari zake kati ya Makumbusho na Bagamoyo kwa vile alikuwa akielekea huko, lakini akashindwa kufafanua jinsi alivyoingia wakati milango na madirisha ya gari hilo yalikuwa yamefungwa.
Hata hivyo, tajiri huyo alifanikiwa kuwasihi wananchi hao kutochukua sheria mkononi, badala yake aliwataka wamuache ili awaite polisi ambao walikuja kumchukua baada ya kuwa amepelekwa katika ofisi ya mradi wa kituo hicho cha mabasi.
Tunguri alizokutwa nazo.
Akisimulia ilivyokuwa, tajiri huyo alisema alikuwa amepitia sokoni ili kununua baadhi ya bidhaa za hotelini na alipofika hapo, alifunga milango yote na madirisha na kuendelea na mambo yake. Lakini alipomwambia kijana wake akalifanyie usafi gari hilo, alishangaa baada ya kuambiwa katika siti ya nyuma, kulikuwa na mtu.
Baada ya kwenda na kumhoji kijana huyo, mara watu walisogea na kutaka kumuua, lakini wao, wakiongozwa na meneja wa hoteli hiyo, Godfrey Hamis walifanikiwa kumuokoa kwa kuomba asipigwe badala yake afikishwe Kituo cha Polisi Kijitonyama (Mabatini).
Gari alilokutwa.
Mwandishi wetu alifika katika kituo hicho cha polisi na kukuta Shaban akiwa mahabusu na polisi wakathibitisha kuwa amefunguliwa jalada la uchunguzi namba KJN/RB/24/2015.