Monday, June 22, 2015

GAIDI JIHADI JOHN ASEMEKANA KUKIMBILIA MAFICHONI LIBYA

Jihad John (kulia) akionekana kwenye video ya ISIS akiwa na mfanyakazi wa utoaji misaada wa Uingereza, David Haines, kabla hajamuua.
Picha za Jihadi John ambaye anasemekana kukimbilia Libya baada ya ISIS kubaini kwamba ametambulika kwa maadui zake.
GAIDI Mohamed Emwazi maarufu kama Jihadi John ambaye ni mpiganaji wa kundi la Kiislam la ISIS anasemekana amekimbilia mafichoni Libya baada ya kufahamika utambulisho wake na kufuatia Taifa la Kiislam kutaka kumuondoa miongoni mwa wapiganaji wake.
Jihadi John akijitayarisha kumchinja mwandishi wa habari wa Marekani, James Foley.
Mpiganaji huyo mwenye umri wa miaka 26, Mwingereza kutoka London, amekuwa akitafutwa sana na Marekani ambayo imelenga makombora sehemu anayofikiriwa kuwa anaishi.
Mwingereza huyo ambaye alitokea katika video za kukatwa watu vichwa, alishukuwa kuwa ameumia vibaya katika mapigano au ameuawa katika mashambulio ya majeshi ya Syria, lakini chanzo kutoka kitengo cha kupambana na ugaidi cha Marekani, kimesema Jihadi amekimbilia Libya.
“Tunafikiri hii ni mbinu ya ISIS ya kumwondoa Emwazi katika nadhari ya watu wanaomtafuta,” alisema ofisa mmoja wa Marekani akizungumza na mwandishi James Fielding wa gazeti la Sunday Express.
Muuaji huyo hajatokea tena katika video za propaganda za ISIS tangu Januari mwaka huu ambapo nyuma alionekana akiwa ameshika kisu akijitayarisha kuwachinja waandishi wa habari wa Marekani, James Foley na Steven Sotloff, mfanyakazi wa utoaji misaada wa Uingereza, David Haines, na dereva Alan Henning wa Salford.
Emwazi alipewa jina la Jihadi John na kundi la mateka waliokuwa wamekamatwa na ISIS.