Wednesday, June 17, 2015

Gari ya kifahari aliyokodi Diamond yazua timbwili mtandaoni, kauli yake yafanya watu wadhani Zari kamnunulia!

Jana Diamond Platnumz alipost picha akiwa kwenye gari ya kifahari na kuandika: Thanks alot baby it’s Finaly Here @zarithebosslady.”
Wengi walitafsiri maneno hayo kama kuwa Diamond anamshukuru Zari kwa kumnunulia gari. Ukweli ni kuwa Diamond alikuwa akimshukuru mchumba wake huyo kwa kuwezesha kupitia connection zake kukodi gari ambalo lingetumika kwenye video ya Yamoto Band inayofanyika Afrika Kusini.
11401228_10207279335086620_2546809343391220504_n
Diamond akiwa na mmiliki wa gari hilo
Kupitia Facebook ambako aliweka picha za mmiliki wa gari hilo akiwa na Diamond, Zari alifafanua kwa kuandika:
Many thanks to ma bro Katsha the king of rides, for making it happen, Ma boo couldn’t stop thanking me I guess it’s always good to have a gal who’s got ya back…. thanks once again. Watch the space # NewVideoTingz.”