Monday, June 22, 2015

Google sasa yakubali kuondoa picha za uchi

Waathiriwa wa picha za ngono katika mtandao wa Google wataruhusiwa kutuma ombi kwa kampuni hiyo la kuziondoa picha hizo, Picha hizo zitaendelea kuwa katika mtandao huo lakini hazitaorodheshwa katika picha wakati wateja watakapozitafuta.

Makamu wa rais wa kampuni hiyo Amit Singhal amesema kuwa mpango huo utashirikisha picha za uchi na zile zenye uchafu mkubwa, Google hapo awali ilikataa jaribio la kuitaka kuondoa picha kama hizo katika picha zilizoorodheshwa katika mashine yake ya utafutaji.


Mpango huo mpya unatarajiwa kuanza kufanya kazi katika kipindi cha wiki chache zijazo