Tuesday, June 23, 2015

KIJANA AJIANDIKISHA MARA MBILI KATIKA DAFTARI LA KUDUMU HUKO KAHAMA, YUKO MIKONONI MWA POLISI

Vitambulisho viwili tofauti vya kijana huy




Mkazi wa Kijiji cha Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga Kefa Eriabu (27)ambaye ni wakala wa mabasi, amekamawata na Jeshi la Polisi kwa kosa la kujiandikisha mara mbili kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kinyume na sheria.


Tukio hilo limetoka leo majira ya saa mbili kamili asubuhi baada ya Mtuhumiwa huyo kutoa vitambulisho hivyo kwa lengo la kuwaonesha wenzake kwamba amefanikiwa kujiandikisha mara Mbili.


Hata hivyo baada ya wenzaka kuona hali hiyo walimhoji kwa nini amejiandikisha zaidi ya mara moja na baadaye walitoa taarifa kwa jeshi la Polisi katika kituo cha Isaka ambao walifika na Kumkamata kwa mahojianao zaidi.




Kijana huyo alijiandikisha kwa mara ya kwanza 18/6,2015 katika kituo cha Isaka Stationi kwa jina la “Kefa D Eriabu kuzaliwa 01/01/1988 na kupewa kadi No T-1004-7969-449-9.


Aidha alifanya hivyo siku ya jumamosi 20/06/2015 katika kituo cha Shule ya Msingi Isaka, wa jina la Kefa D Jonhson amezaliwa 10/05/1995 na kupewa kadi no,T-1004-4564-460-3.


Dunia Kiganjani Blog ilifanikiwa kuzungumza na kijana huyo ambapo alikiri kufanya hivyo kwa lengo la kuhofia kupoteza kitambulisho na wala hakuna aliyemtuma kufanya hivyo.


“Ni kweli mimejiandikisha mara mbili ila sikujua kama ni kosa, nilifanya hivyo kwa hofu ya kupoteza kitambulisho na ndio maana nilifika kazini nikawaeleza wenzangu sijui ilikuwa ni mtego”alisema Kefa.


Hili ni tukio la kwanza kutokea katika wilaya ya Kahama, na ni siku tatu tangu kijana mwingine akamwatwe mkoani Mbeya kwa kosa kama hilo.


Jeshi la Polisi wilayani Kahama linamshikilia kwa mahojiano zaidi na upelelezi utakapokamiliaka atafikishwa mahakamani