Monday, June 15, 2015

MAKUBWA:Yule Gavana aliyeoa binti mdogo.. Afunguka Mazito Hii Ndiyo Siri Ya Mapenzi Yao

 
Gavana wa jimbo la Edo la nchini Nigeria, Adams Oshiomhole, amemuelezea mke wake, Iara, kama
mlimbwendwe kwenye moyo wake na kwamba si kwamba hajamuoa kuziba pengo la mke wake
aliyefariki. Akiongea kwenye misa ya shukrani kwenye kanisa la Immaculate Conception Cathedral, Auchi, Jumapili iliyopita, Oshiomhole alizipuuzia ripoti kuwa mke wake ni model maarufu na kudai kuwa maneno hayo yametokana na urembo wa mke wake. “Ninaposoma habari za kwenye magazeti na wanasema kuwa Comrade ameoa ‘mlimbwende’ mimi nasema labda ni mtu mwingine,” alisema.
“Msichana ambaye Mungu amleta kwangu kumuoa hakuwahi na si mlimbwende. Of course, ni
mrembo na naelewa kwanini watu wanadhani msichana wa aina hii anaweza kuwa model, of
course, ni model moyoni mwangu na tuna tumaini na kuomba kwenye moyo wa Mungu wetu na
nadhani hicho ndio kitu muhimu.” Gavana huyo ana umri wa miaka 63 huku mke
wake huyo mpya ana miaka 36. Mrembo huyo ni raia wa Cape Verde na alifunga naye ndoa weekend
iliyopita. Ndoa yao ilifungwa mbele ya wageni akiwemo rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na mtu tajiri zaidi Afrika, Aliko Dangote. Ndoa hiyo imekuwa gumzo kwenye bara zima la
Afrika.