MAONESHO ya biashara ya kimataifa yameanza jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (zamani vikiitwa Saba Saba) vilivyoko Barabara ya Kilwa ambako makampuni na taasisi zinaonyesha bidhaa zake.
Uzinduzi rasmi wa maonyesho hayo utafanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Julai 3 mwaka huu.