Friday, June 19, 2015

Mimi nikipata management kama ya Diamond nitakuwa mbali sana – Christian Bella

Christian Bella ni muimbaji anayeamini kuwa ili msanii afanikiwe zaidi anahitaji kuwa na management nzuri.

Muimbaji huyo wa ‘Nashindwa’ ameisifia management ya Diamond na kuongeza kuwa endapo angeweza kuwa na watu imara wa kumsimamia angekuwa mbali zaidi ya hapo alipo.


  • “Mi napenda kusema ukweli, Diamond yuko vizuri na management yake wanajitahidi vizuri, yeye msanii akiwa na management nzuri yaani Babu Tale na Fella nawapa bigup sana.”Alisema Bella kupitia 255 ya Clouds Fm. “Ndo tunataka watu kama wale wawepo, mimi nikipata watu kama wale wee! itakuwa mbali sana kwasababu mimi najua kwamba mimi ninauwezo wa kuimba nina vocal najua melody za kuimba, ila nakosa tu watu wa kukunyanyua, kwamba lala usingizi tunaenda kuongea na Fally Ipupa, we lala yaani zima simu wanakwambia we studio kesho, aah yaani naenda nauwa, ndo wasanii wa mbele wanaishi hivyo.” alimaliza.


Kuhusu wasanii ambao anatamani kuja kufanya nao collabo akipata nafasi, Bella amesema kwa Marekani anatamani kuja kufanya kazi na Chris Brown, na kwa Afrika anatamani kuja kufanya kazi na Fally Ipupa, P-Square na Wizkid.