Friday, June 5, 2015

Tamaa ya Kuwa na MAKALIO Makubwa Yamsababishia Kifo Msichana Huyu Mrembo

Ishu ya wasichana na wanawake kupenda
kuongeza maumbile ya miili yao limekua kama
ishu ambayo imechukua sana nafasi sehemu
mbalimbali duniani.
Tunashuhudia watu wengi wakiongeza makalio
kwa kusudi la kuwa wenye mvuto zaidi, na
kumekuwepo na vidonge na sasa kuna sindano
za kuongeza makalio.
Leo nimekutana na stori iliyotokea Los Angeles
Marekani, ambako msichana Kelly Mayhew
mwenye miaka 34 amefariki baada ya
kufikishwa St.John’s Espiscopal Hospital, muda
mfupi baada ya kuchomwa sindano ya
kuongeza makalio.
Kelly Mayhew na mama yake walisafiri kutoka
Maryland kwenda Rockaway, walikokua
wameelekezwa na rafiki yake Kelly ili kwenda
kuchoma sindano hiyo ambayo ilikua inatolewa
kinyume na utaratibu… mtoaji wa huduma hiyo
alijiita daktari lakini hakuwa amesajiliwa na
alikuwa hatambuliki kisheria.
Baada ya kuchomwa sindano hiyo, Kelly alianza
kupumua kwa shida, akawa anajitupa ovyo
chini huku akiishiwa pumzi… baada ya
kuhangaika kwa kama dakika ishirini hivi, Kelly
alifariki akiwa kwenye mikono ya mama yake..
mpaka Polisi wanafika eneo hilo Daktari
alikuwa tayari kashakimbia.