Kwenye video iliyosambaa kwenye mtandao anaonekana Xavi akimsukuma usoni Neymar wakiwa kwenye hilo bus. Video hiyo imetafsiriwa kwamba kulitokea ugomvi kati ya wachezaji wakiwa kwenye sherehe za zao.
Lakini Xavi amesema kwanini alifanya vile. Kwenye maelezo yake alisema hivi, “Pale ndani ya basi tukiendelea kusherekea walijaribu kunisukuma kwenye wakati nikiwa kwenye pembe ya basi. Wakiendelea kufanya hivyo walikua wanajaribu kunivua viatu. Unaweza kunywa bia lakini inabidi usiende juu zaidi ukapitiliza. Bus parade ni sehemu ya mashabiki kufurahia na sio vinginevyo.”
Kinachoonekana hapa ulikua ni utani ambao Xavi aliona umepitiliza na ukamshinda.Kama video ilikupita ni hii hapa.