Friday, July 17, 2015

AUNT AWATIBUA WAISLAM, SHEHE AMVAA!

arobainiAunt Ezekiel akiwa na watoto.
WAANDISHI WETU
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ambaye jina lake la Kiislam baada ya kubadili dini ni Rahma, hivi karibuni alifanya maulidi ya kumtoa mwanaye Cookie lakini katika hali ya kushangaza alifanya mambo ambayo yaliwatibua Waislam, Ijumaa lina ishu nzima.
Ilikuwa nyumbani kwake
Aunt alifanya tukio hilo hivi karibuni nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar kisha kuwaalika ndugu, jamaa na marafiki ambapo mbali na kuombewa dua na maustadhi, pia aliwafuturisha Waislam waliokuwa kwenye mfungo.
Licha ya kitendo hicho kilichodaiwa kuteketeza milioni kadhaa za fedha kupongezwa na wengi, katika hali ya kushangaza kuna mambo ambayo ilibainika yalikwenda kinyume na taratibu za dini ya Kiislam.
auntzShughuli nzima ilivyokuwa.
Kwanza
Aunt baada ya kutokea kwenye hadhara akiwa na mwanaye, alikuwa kavalia shela lilioacha wazi sehemu ya juu ya kifua na kimtandio ambacho baadaye kiliondoka na kumuacha kichwa wazi, kitu ambacho ni kinyume na Uislam.
Pili
Katika tukio hilo kulikuwa na ratiba ya kukata keki ambapo ulipofika muda wa yeye kumlisha mwanaume aliyezaa naye (Moze Iyobo), alimpa kwa staili ya ‘njiwa’,  jambo ambalo halikutarajiwa kufanyika katika mazingira yale.
Tatu
Mjadala mwingine ulihusu Aunt  kugandana na Moze Iyobo kama mume na mke wakati mtoto huyo wamempata nje ya ndoa.
Baada ya tukio hilo, baadhi ya Waislam waliozungumza na Ijumaa walishangazwa na kile alichokifanya staa huyo na kueleza kuwa hakikustahili kufanyika katika mazingira yale.
“Ile kudendeka mbele yetu tena ndani ya mwezi mtukufu halafu na mwanaume ambaye siyo mume wake, ilikuwa kitu kibaya.
“Halafu lile vazi nalo halikuwa la kuvaliwa pale, hivi hakuona wanawake wenzake walivyokuwa wamejitanda? Kimsingi hakufanya sawa,” alisema Rashid Selemani ambaye ni mmoja wa vijana waliohudhuria.
Shehe amvaa
Baada ya kuona na kusikia malalamiko ya baadhi ya wageni waalikwa kuhusu sherehe hiyo, gazeti hili lilimtafuta Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar, Alhad Mussa Salum ambaye alionesha kushangazwa na jambo hilo na kusema ni makosa na kufanya hivyo ni kuchezea dini ya Mwenyezi Mungu.
“Mtu anayefanya mambo hayo ni kwamba huko ni kuchezea dini ya Mwenyezi Mungu, watu wanatakiwa kuelewa kwamba utukufu wa Mwezi wa Ramadhani ni usiku na mchana. Kama kuna staa kafanya hivyo, amemkosea sana Mungu,” alisema shehe mkuu.