Thursday, July 9, 2015

HAYA NDO MAGARI YA KUMPOKEA OBAMA NCHINI KENYA YAKIWASILI NA NDEGE TOKA MAREKANI

2000
Zimebaki kama wiki mbili hivi ugeni wa White House utue pale Jomo Kenyatta International Airport, Nairobi Kenya kama ambavyo iliahidiwa.
Safari ya kihistoria ya Rais Obama ndani ya Kenya inakaribia, huu ni uthibitisho mwingine kwamba mambo yameiva… Gari za watu wa Usalama tayari zimeshushwa Nairobi na pia kuna Helicopter zaidi ya nane za Kijeshi tayari zimetua.
12
Mbali na gari hizo pamoja na helicopter zilizotua, wako Maofisa Usalama zaidi ya 200 ambao tayari wako Kenya kwa ajili ya kuhakikisha mpaka siku Rais Obama anatua kunakuwa na usalama wa kutosha.
12_0
Stori nyingine kutoka Nairobi inaonesha timu ya watu wa Usalama watakuwa kama 800 hivi kutoka Marekani na Polisi zaidi ya 2,000 wa Kenya watahusika na Ulinzi wa msafara wa Obama akiwa Kenya.
BO UK
Marine One helicopter, carrying US President Barack Obama, prepares to land next to the Presidential limousine, known as "The Beast," at the Wall Street landing zone in New York City, March 11, 2014, prior to attending Democratic fundraisers and stopping at a Gap clothing store to highlight his proposal to raise the federal minimum wage. AFP PHOTO / Saul LOEB        (Photo credit should read SAUL LOEB/AFP/Getty Images)
‘The Beast’ ya Rais Obama na Helicopter juu vitakuwa Nairobi time yoyote kuanzia sasa hivi.