Sunday, July 5, 2015

MEYA JERRY SILAA AACHA SIMANZI ILALA,WANANCHI WAMLILIA..AOMBA KUGOMBEA UBUNGE UKONGA

Diwani wa kata ya Gongolamboto na Meya wa manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Mhe.Jerry William Silaa akielezea mafanikio ya ahadi alizotoa katika manispaa ya ilala tangu alipochaguliwa kuwa meya mwaka 2010 hadi 2015 ambapo ameelezea mafanikio makubwa katika sekta ya afya,elimu na uchumi kwa wananchi wa Manispaa hiyo ambapo ni mwendelezo wake wa  ziara yake ya kuwaaga wananchi wa manispaa ya ilala ambapo jana amefanya mkutano mkubwa wa Hadhara ulioudhuriwa na maelfu ya wananchi wa ukonga na ilala.

Naye Mbunge wa Temeke Mhe.Abbas Mtemvu akihutubia wananchi wa ilala katika mkutano huo ambapo moja ya mambo aliyowaambia ni kwamba Ilala haijawahi kupata meya mwenye upeo mkubwa na kingozi bora kwa muda mfupi kama Jerry
Mtemvu alisema''...Manispaa ya Ilala na Dar es Salaam yote hakuna ansiyejua utendaji wa Jerry Silaa..''naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mhe.Adam Kimbisa alisema,Jerry ni kijana wa mfano wa kuigwa katika siasa za nchi hii inayohitaji wanasiasa wenye kutekeleza malengo kwani siasa za sasa zinahitaji kutekeleza ahadi na siyo tu kuahidi kama mazoea yalivyo kwa viongozi wengi,huku akiwaomba wananchi hao kumuunga mkono wa dhati katika lengo lake hilo la kugombea ubunge jimbo la ukonga katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwani tayari ameonyesha uwezo mkubwa wa kuismsmia manispaa ya iala...
Hii ni sehemu ya wananchi wa ukonga na ilala waliofika Katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kitunda iliyoko eneo la ukonga jijini Dar es Saam ambapo muda wote wa mkutano huo alikuwa akishangiliwa na wananchi waliofurika kwa wingi kumsikiliza.