Sunday, July 5, 2015

Jerry Muro, Kwa Kiingereza chako hiki, hakika umejidhalilisha na kuwatia aibu mno Walimu wako wote

Akiwa Anazungumza Kwa Madaha Katika Kituo Cha Magic FM Kipindi Katika Kipindi Chao Cha MICHEZO Huku Muda Mwingi Akitumia Kuiponda Simba Na Haswa Viongozi Wake Na Haswa Akimlenga Msemaji Mwenzie Haji Manara Kuwa Hajui Kuongea Kiingereza Na Ndiyo Maana Simba Haiendi Mbali Kusajili Wachezaji Anaowaita Yeye " Wa Kimataifa " Na Wanaishia Tu Kusajili Wachezaji Wa Nchi Za Karibu Wanaoongea Kiswahili ( Hapa Akimaanisha Wa Uganda, Kenya Na Burundi ).

Baada Ya Hapo Jerry Muro Nae Tena Mbele Ya Waandishi Wa Habari Akazungumza Kiingereza Hiki Nitakachokiandika Hapa Na Alichokuwa Anataka Kumaanisha Kisha Tutajua Je Ni Kweli Anajua Kiingereza au Ni Wale Wale? Halafu Hapo Hapo Anasema Kuwa Ana MASTER'S DEGREE Ya Public Administration Lakini Hatuambii Kasoma Lini, Wapi Na Kamaliza Lini Na Huku Akiwa Amesahau Kuwa Wapo Watu Wanaomjua A To Z au KINDAKINDAKI Kuliko Hata Anavyojijua Yeye ILA Tumeamua Tu Kumfichia Siri Kwa Kumuheshimu Kwakuwa Tu Ni Mwana Tasnia Mwenzetu.

Kiingereza Chake Ni Hiki kifuatacho Na Nitaomba Sana Kama Huna Background Nzuri Ya Kiingereza SANIFU Tusipotezeane Muda Kwa Kubishana Bali Nataka Watakaochangia Basi Wawe Kweli Ni Wazuri Ktk Communication Skills Na Matumizi Ya Lugha Yenyewe Ambayo Msemaji Wa Yanga Jerry Muro Anasema Anaijua Huku Akidai Viongozi Wa Simba Hawakijui.

Yanga Tuko Vizuri............Yeye Akasema............Yanga We Are Much Okey.
Yanga Tuko Tayari..........Yeye Akasema............Yanga We Are Arleady.

Wataalam Wa Lugha, Wajuvi Wa Kiingereza Cha Kuzungumza Na Kuandika Na Hata Wale Mliosoma Vizuri Sana Communication Skills Naombeni Mnisaidie Je Kusema " Yanga We Are Much Okey " Na " Yanga We Are Already " Ni Kiingereza Sahihi Na Ambacho Mtu Wa Caliber Ya POPOMA Jerry Murro Anaweza Kujivunia Nacho?

Na Namalizia Tu Kwa Kumkumbusha Jerry Muro Kuwa Msemaji Mwenzie Wa Simba Sports Club Haji Manara Ni Msomi ALIYETUKUKA Vizuri Tu Na Haishii Tu Kuongea Kiingereza Kizuri Lakini Kwa Faida Yake Na Wengine Msiojua Haji Manara Pia Ni Linguist Tena ALIYETUKUKA.
JF