Saturday, July 11, 2015

MKE AFUMANIA, ACHEZEA KICHAPO!

Mashaka kisusi
NDANI ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mama mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, mkazi wa maeneo ya stendi, wilayani Misungwi mkoani Mwanza anadaiwa kuchezea kichapo kutoka kwa mumewe baada ya kumfumania akiwa na kimada, Risasi Jumamosi linatiririka.
Akivuja damu baada ya kuminyiwa kichapo.
Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilijiri mwanzoni mwa wiki hii ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, awali mwanamke huyo alipita maeneo hayo akiwa anaongea na mtu kupitia simu yake ya mkononi, lakini baada ya muda alirudi akiwa analia huku damu chapachapa.
“Alitonywa kwa njia ya simu kwamba mumewe yuko kilabuni na kimada, ndipo alipomuibukia lakini nasikia mumewe kakolea kwa huyo kimada, hivyo akamgeuzia kibao kwa kumtaka aondoke. Alipogoma sasa ndiyo akalazimika kumpa kichapo hevi hadi kumtoa damu,” alisema shuhuda huyo.
Akizidi kupewa kichapo na mumewe.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, baada ya kichapo hicho, mwanamke huyo alitimkia kwenye stendi hiyo ambapo wasamaria wema walimpa msaada baada ya kumuona anavuja damu usoni lakini alipoulizwa kulikoni, alikataa kuzungumzia fumanizi hilo kwa undani na kutaka arudishwe kwa mumewe akalipe kisasi.
“Nirudisheni! Nirudisheni! Nasema nirudisheni kule  nikalipe kisasi, sikubali,” alisikika akisema mwanamke huyo huku akiangua kilio.
Hata hivyo, wananchi wenye maneno ya faraja walimtuliza kwa kumwambia asirudi ili asipatwe na majanga zaidi kisha wakamshauri aende nyumbani kwake kuepusha shari, ushauri ambao aliuafiki na kukubali kurudi nyumbani kwake.