TUHUMA za ushirikina zinaendelea kumganda staa wa filamu Bongo, Ester Kiama anayedaiwa kujipandisha kisanaa kwa nguvu za giza zinazotokana na kitendo chake cha kuvaa pete yenye kito cha bluu.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha habari, baadhi ya wasanii wenzake wamekuwa wakimsengenya kuwa pete yake hiyo amekuwa akiivaa muda wote, hata akiwa bafuni, kitendo kinachowafanya wahisi ni nguvu za giza, kwani hata akiambiwa aivue wakati wakiwa ‘location’ amekuwa akikataa.
Lakini Ester alipozungumza na gazeti hili, alikana suala hilo, akidai kuchoshwa na maneno dhidi yake, kwani kinachowasumbua ni wivu wa kumuona akija juu, kitu alichosema hakimtishi kwani ipo siku watatambua upande wake wa pili wa maisha.